• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

Mfuko wa Jimbo Rufiji ulivyopunguza adha ya Wanafunzi kutembea umbali wa km7 Kufuata Shule Muhoro.

Posted on: February 19th, 2024

Yametimia. Ile shida na tabu iliyokuwa inawatesa Wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza ya kutembea umbali wa takribani Kilomita 7 kutoka kitongoji cha Nyandote (mashambani) Kijiji cha Muhoro Mgharibi mpaka shule ya Msingi Muhoro ,kata ya Muhoro Wilayani Rufiji Mkoani Pwani sasa imekwisha baada ya kujengewa kituo shikizi cha Haidali chenye madarasa mawili, ofisi na matundu ya vyoo kupitia Mfuko wa jimbo la Rufiji.

Shughuli kubwa ya Wakazi wa eneo hilo ni kilimo cha Mahindi, mpunga, ndizi pamoja na Ufugaji.

Tatizo la umbali mrefu kwa watoto wadogo  liliigusa mfuko wa jimbo la Rufiji ambao upo chini ya Mbunge Mhe. Mohamed Omary Mchenhgerwa kwa kujenga shule shikizi ya Haidali yenye madarasa mawili, ofisi na matundu sita ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 38.6 kwa ajili ya kuwapunguzia adha watoto hao ambao wengi wao ni darasa la awali na darasa la kwanza.



Akizungumzia namna mfuko wa jimbo  ulivyoigusa jamii hiyo baada ya kamati ya mfuko wa jimbo kuitembelea shule, Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo Hassan Mpange, amesema mpaka sasa shule imeshakusanya Wanafunzi 90 wa darasa la kwanza na Wananfunzi 40 wa darasa la awali.

“shule ya Haidali leo imekamilika, leo Wanafunzi Wanasoma, hawaendi umbali mrefu ambao mwanzo walikuwa wanatembea umbali wa kilometa 7” amesema.

Ameongeza kuwa ujenzi wa madarasa hayo ilikuwa ni ushawishi wa Mbunge wa jimbo la Rufiji ambaye sasa ni Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa baada ya kuona Wanafunzi wanapata shida ya kutembea umbali mrefu.

Wanafunzi katika Kitongoji hicho walikuwa wanalazimika kuvuka mabonde ya maji na kupita sehemu zenye miinuko mpaka kufika shule ya Msingi Muhoro.

Mwenyekiti Muhoro Mashagharibi azungumza.

Akisimulia mchakato ulivyoanza wa kuianzisha shule hiyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Muhoro Magharibi Amini Ally Mnyimwa amesema shule hiyo iliibuliwa na Jumuiya ya Wazazi CCM baada ya kuona Wanafunzi wanatembea umbali mrefu, hivyo lilifanyika kongamano la kuhamashisha ujenza wa shule hiyo na viongozi mbalimbali waliunga mkono na kutoa michango yao.


“viongozi mbalimbali walitoa ahadi zao kwenye kongamano na ahadi zao zilikamilika, tukaanza huu mchakato kama Halmashauri ya serikali ya kijiji, tulichimba msingi mpaka katika hatua ya jamvi” amesimulia Mnyimwa.

Aliongeza kuwa masikitiko yao waliyepeleka katika mfuko wa jimbo ambapo ndio wameimaliza tatizo hilo na sasa Wanafunzi wanasoma.

“mara ya kwanza tulipokea milioni 26, 500,000 baada ya hapo kukawa na mapungufu ya umaliziaji wa hili jengo tukaongezwa tena milioni 12, 000,000” aliongeza.


Mbali na hayo amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Rufiji na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa juhudi za ujenzi wa shule hiyo.

“tunaushukuru sana mfuko wa jimbo na Mbunge Mchengerwa kwasababu unapotawala watu lazima uweke alama” alisema.

Mbali na hayo pia Mnyimwa alizitaja baadhi ya changamoto ya shule hiyo kuwa ni madawati, meza na viti vya Walimu, Walimu, Kisima cha maji na barabara.

Awali Makamu Mwenyekiti wa mfuko wa jimbo wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Hassan Mpange aliwashauri Wazazi kutuma maombi ya changamoto zilizopo katika shule hiyo na waziwasilishe katika mfuko jimbo ili ziweze kufanyiwa kazi.

Mtendaji Kata ya Muhoro azungumza.

Kwaupande wake Mtendaji kat ya Muhoro ambaye akizungumza kwa niaba ya Diwani wa kata hiyo Hilda Kuboja alisema mfuko wa jimbo Wilya ya Rufiji imegusa katika kila kijiji kati ya vijiji 6 vilivyopo kata ya Muhoro.

“shule hii ya Haidali kwa asilimia 95 imejengwa na mfuko wa jimbo, ulileta shilingi 38, 600,000 milioni ambayo imemaliza madarasa mawili, ofisi na matundu 6 ya vyoo. Watoto walikuwa wanatembea umbali mrefu mpaka kufuata shule nyingine na hapo katikati kuna mabonde na madimbwi ya maji kwahiyo wale watoto wadogo walikuwa wanabaki majumbani” alisema Kuboja.

Amesema hiyo ilikuwa inachangia Wanafunzi kuanza shule wakiwa na umri mkubwa kutokana na hali ya hewa na hali ya barabara.

“lakini kuwepo kwa shule hii iliyoasisiwa na Mbunge (Mchengerwa) mpaka sasa tunao wanafunzi wa darasa la kwanza 90 ambao wameandikishwa kwenye shule hii na Wanafunzi wa darasa la awali 40.

Tunashukuru sana kwa namna shule hii ilivyokuwa msaada” ameshukuru.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA RUFIJI WAANZA MAFUNZO RASMI

    August 04, 2025
  • PINDA AZINDUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI MKOANI MOROGORO

    August 02, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa