• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

KAMATI YA SIASA RUFIJI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: July 13th, 2024

Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Rufiji, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali huku ikionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo, ukiwemo ukarabati wa majengo chakavu ya hospitali ya Wilaya ya Rufiji (Utete) inayo inagharimu milioni 900 kutoka serikali kuu.


"ukarabati huo unahusisha, jengo la Wagonjwa wa nje, jengo la upasuaji, jengo la maabara, jengo la wodi ya Wanawake, jengo la CTC, jengo la kifua kikuu, jengo la huduma ya Afya, mama na Mtoto, jengo la Wazazi, pamoja na ukarabati wa korido" alibainisha Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Dkt. Hamis Abdallah wakati akisoma taarifa kwa Kamati ya siasa ya Wilaya.


Amesema ujenzi huo utakapokamilika utasaidia kubadili mandhari ya hospitali kuwa ya Kisasa na kuongeza morali ya Watumishi kufanya kazi.


Ziara hiyo imefanyika leo Alhamisi  Julai 13, 2024, iliyolenga kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Wilaya ya Rufiji ambapo Kamati hiyo ilimpongeza Mkandarasi kwa namna anavyoendelea kujenga kwa viwango huku wakimtaka aongeze kasi.


"hii sehemu ni sehemu muhimu sana kwa maisha ya Wanadamu, kwahiyo ni vizuri ukaongeza kasi ili Wananchi wapate huduma" alisema Rajabu Mbonde Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rufiji.


Mradi Mwingine walioukagua ni mradi wa jengo la Mama, Baba na Mtoto lilijengwa katika Kijiji cha Mbwara Kata ya Mbwara lenye thamani ya Shilingi milioni 50 kutoka mapato ya ndani.


Pia walikagua ujenzi wa Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Chumbi inayojengwa Kijiji cha Chumbi A,yenye thamani ya shilingi milioni 30 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.


Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele, alitumia ziara hiyo kuwataka Mafundi ambao ni Wazawa wa Rufiji kuendelea kujifunza kwa Wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali ya serikali, ili kuongeza ubunifu na kiwa bora zaidi.


Vilevile Kamati hiyo ilikagua Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Mohoro inayojengwa katika Kijiji cha Kiwanga yenye thamani ya shilingi milioni 529, ambao utasaidia kuwapunguzia adha Wanafunzi zaidi ya 400 kwenda kufuata shule umbali mrefu Mohoro Sekondari.


Mbali na miradi hiyo, walitembelea mradi wa Shule shikizi Kindwitwi ikiyopo katika Kitongoji cha Kindwitwi Kata ya Chemchem ambayo itasaidia Wanafunzi na Wakazi wa Kata ya Chemchem ya kupunuza adha ya kutembea umbali mrefu kufuata shule.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa