• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

DC SAWALA NA MCHENGERWA WASIKILIZA KILIO CHA WAKULIMA WA UFUTA NA KOROSHO RUFIJI.

Posted on: January 8th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni kanali Patrick Sawala ameungana na Mhe. Mohamed Mchengerwa Mbunge wa Rufiji, kusikiliza kilio cha Wakulima wa zao la ufuta na korosho Wilayani humo juu ya kutokuwa na imani na chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani ( CORECU) na kueleza dhamira yao ya kujitoa katika chama hicho ili kuunda kingine kitakacholeta ushindani na kupelekea kuboresha maslahi ya Wakulima wa mazao hayo.Akizungumza na Wakulima hao, Sawala amesema hakuna sababu ya Wakulima kukata mikorosho yao na kubadilisha aina hiyo ya kilimo badala yake uongozi wa Wilaya utayafanyia kazi malalamiko yao. “ Hakuna sababu ya kukata mikorosho shambani kwa sababu ya kushuka kwa bei ya zao hilo, korosho ni dhahabu ya kijani na Mvumilivu hula mbivu. Zile korosho zitatutoa. Mimi nitashirikiana na viongozi wenzangu kuhakikisha tunapata ufumbuzi wa changamoto hizi.” Alisema.Pia amewataka Viongozi wa vyama vya msingi wanaodaiwa na Wakulima kuhakikisha wanalipa fedha za wakulima vinginevyo mali zao zitataifishwa.”Ninawataka viongozi wa vyama vya msingi vinavyodaiwa kulipa fedha za Wakulima vinginevyo tutataifisha kilakitu.”Alisema.Sambamba na hilo amewataka maafisa kilimo kuwasaidia Wakulima kwa moyo pamoja na chamgamoto wanazopitia na kuiomba halmashauri kuchukua hatua za makusudi kuwanunulia pikipiki maafisa kilimo kata ili kurahisisha utendaji wao kwa wakulima katika kata zao..”Ona moyoni mwako kuwa unawajibika kuwasaidia wakulima pamoja na changamoto mnazopitia.” Alisema.Aidha Sawala amewataka wakulima hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kuhakikisha kuwa wanaongeza vyama vya msingi ili kuwa na vyama vya ,msingi vingi vitakavyowezesha kukidhi vigezo na kuleta ushawishi wa kuunda chama kingine kinatakachoipa CORECUchangamoto. “ mimi pia sifurahishwi na namna ambavyo CORECU inaendesha mambo yake. Hatuna sababu ya kutoanza minada ya korosho kwa wakati pindi Korosho zetu zinapokuwa tayari, Suala la vifungashio kununua nje wakati tunaweza kutumia viwanda vyetu vya ndani. “ AlisemaNaye Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mbunge), amesema kuwa, umefikia wakati Rufiji kuamua kujitoa na kuungana na Wilaya za jirani kuunda ushirika mwingine ili kuepukana na malalamiko mengi sana ya Wakulima yanayosababishwa na CORECU. “ Hatuwezi kukubali kuendelea na CORECU kwani ina malalamiko mengi sana ambayo ni aibu hata kwa serikali yetu ambayo inafanya jitihada kubwa kuwasaidia wakulima. Muda umefika tumeamua kujitoa. Tukitoka tukaanzisha chama chetu kingine tutaweza kuongeza ushindani na tutafanya vizuri. Serikali itaongeza mapato na wakulima wataneemeka. Afisa Ushirika naomba shughulikia hilo, pale ambapo tutashindwa mimi nitakwenda mpaka kwa Mrajisi Mkuu. Hakuna sababu ya kuzuiliwa.” Alisema.Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Muharami Mchambwa(Diwani) amesema kuwa atalipeleka katika baraza ombi la kununua pikipiki za Maafisa kilimo kata ili kuboresha huduma kwa Wakulima.Awali, Wakulima walipewa nafasi ya kutaja kero zinazowakabili na kuwafanya wawe katika hali ya kukata tama na kupendekeza suluhisho la kero hizo ambapo walisema kutokana na matendo ya dhuluma za ukatwaji wa tozo zisizofahamika ambazo wanadai mpaka leo, kuwepo kwa mkanganyiko wa upimaji wa ubora wa korosho uliojitokeza kwa Wataalamu wengine kusema bora na wengine kuweka katika kundi B, kutokuwepo kwa usimamizi mzuri wa ghala kuu, utafutwaji masoko wenye vuashiria vya upendeleo pamoja na kuchelewa kwa vifungashio kwa baadhi ya maeneo na kwengine kuwahi badala ya kugawiwa sawa. Kunawanyima imani ya kuendelea na ushirika huo na kupendekeza kujitoa katika ushirika huo ili kujipanga kuunda ushirika mwingine mapema ili kuwahi msimu wa zao la ufuta.Pia wamemuomba Mkuu wa Wilaya pamoja na Mbunge kuwasaidia kufikisha muhtasari wa kikao chao kwa Mamlaka za juu ikiwemo kwa Mkuu wa Mkoa ilikuona adhma yao na kupatiwa msaada.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

    May 16, 2025
  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa