• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

DC: GOWELE: MAZINGIRA NI UHAI WETU, NI LAZIMA TUPANDE MITI LAKINI PIA TUITUNZE

Posted on: April 1st, 2022


Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amewataka Wananchi wa Wilaya ya Rufiji kuhakikisha Wanayatunza mazingira kwa kupanda miti na kuitunza badala ya kukata miti ama kuichoma moto hususani wakati wa maandilizi ya mashamba.
Meja Gowele ameyasema hayo leo Aprili 1. 2022 wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti Kitaifa ambapo kiwilaya yamefanyika katika shamba la miti la Halmashauri lililopo katika Kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwara Wilayani humo.
“ Mazingira ni uhai wetu, mazingira yakiwa mabaya hatuwezi tukawa salama kwahiyo ni lazima tupande miti na kuitunza.” Alisema Gowele.
Pia amepongeza jitihada za Halmashauri kumiliki shamba la miti hekari 100 na kuliendeleza kwa kupanda miti takribani 3000 swala alilolitaja kuwa ni mfano wa kuigwa na Wananchi katika vijiji vyao Wilayani humo.
Sambamba na hilo, ametoa msisitizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha agizo la kila mwananfunzi kuwa na mti anaouhudumia shuleni linatekelezwa kwa umahiri Mkubwa huku akisistiza upandaji wa miti ya matunda katika taasisi za Serikali.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Afisa Misitu Wilaya ya Rufiji Augenia Majura Seleman alisema  katika kuazimisha siku ya upandaji miti kitaifa, Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ,  imepanda jumla ya miti 3000 katika shamba la miti lenye ukubwa wa hekari 100 linalomilikiwa na Halmashauri katika Kijiji hicho.  
“ katika jitihada za kurejesha uoto uliopotea kutokana na shughuli za binadamu, Wilaya ya Rufiji  inaendeleza jitihada za kuhakikisha inapanda miti katika hekari zote 100.” Alisema 
Aliongeza kuwa, lengo la kushirikisha wanafunzi katika zoezi la upandaji  miti ni kuwa Wanafunzi ni Taifa la kesho, hivyo ushiriki wao katika kupanda miti itawajengea uelewa na uwezo wa kutambua umuhimu wa kuhifadhi misitu na kutunza mazingira kwa ujumla na kutengeneza kizazi ambacho kitaweka jitihada kuthamini utunzaji wa mazingira.
Maadhimisho hayo yalishereheshwa  na washiriki toka  Kamati ya Usalama ya Wilaya, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri na Wataalamu toka Idara za Halmashauri, wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS), pamoja na kamati ya maliasili kijiji cha Nyamwage, shule ya msingi Nyamwage na Shule ya Sekondari  Nyamwage huku yakiwa yamepambwa na kauli Mbiu isemayo; “Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, kazi iendelee.”

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA RUFIJI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI, WASISITIZWA KUFANYAKAZI KWA BIDII, WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA UPENDELEO MAOFISNI

    June 25, 2025
  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa