• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

DAWA YA PANYA WAHARIBIFU RUFIJI YAPATIKANA

Posted on: November 25th, 2023

Kutokana na Malalamiko ya Wakulima Wilayani Rufiji Mkoani Pwani juu ya Panya kufukua mbegu ya Mahindi kila kukicha, sasa tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi baada ya dawa aina ya ‘ZINK FORCE FID’ kugaiwa leo kwaajili ya kupunguza tatizo hilo.

Dawa hiyo iliyochanganywa na pumba za Mahindi, dagaa, pamoja na mafuta imegaiwa leo Novemba 24, 2023 katika ofisi ya Mtendaji Kata ya Utete na kusambazwa maeneo mbalimbali Wilayani Rufiji.

Akizungumza na Wananchi Ramadhani Mahuna, Afisa Kilimo Msaidizi Mwandamizi Kitengo cha Kudhibiti Baa la Panya Morogoro sumu hiyo ni kwa ajili ya Panya wa Mashambani huku akiwataka Wakulima waliopata dawa hiyo kupanda wote kwa pamoja.

“hii sumu ni kali inaua kwa njia ya gesi, kwahiyo unaiweka kidogo kwenye mfuko laini alafu unaifunga, alafu hivi vifuko unavitupa mashambani, hawa panya wakisikia hii harufu ya dagaa wataipenda, sasa wakila ndo inawaua”

Kwa upande wake  Afisa Kilimo Rufiji Nurudin Mkumbugo amesema dawa hiyo ni vizuri iwekwe mashambani wakati wa jioni kuelekea usiku kwa sababu ndio mida ya Panya kufukua Mahindi mashambani.

“mashambani tunaweka kwa namna gani, kama hali ya hewa unaona kama mvua hakuna au unyevu ni mkubwa na tumepangilia labda tuiweke kesho, basi  lazima hii sumu iwekwe kwenye mifuko laini, uhakikishe haiwezi kupitisha hewa wala kutoa hewa kwasababu inaua kwa njia ya gesi maana yenyewe itakuwa inapumua” amefafanua Mkumbugo.

Wakizungumza baada ya kupokea dawa hiyo ya kuulia Panya Mashambani Wananchi akiwemo Zainabu Ndambwe Mkazi wa Kitongoji cha Kiwili Kata ya Utete, ameishukuru Serikali kwa juhudi ilizozichukua baada ya kupokea kero hiyo kwa Wakulima.

“naishukuru Serikali kwa kutuletea Wataalamu wetu kutugea elimu, tumeikubali elimu hiyo na tunaenda kuifanyia kazi” amesema Ndambwe.

Akielezea tabu Wanayoipata Mashambani kutoka kwa Panya hao, Ndulu Kirungi amesema kila wanapopanda Mahindi, panya huwa wanafukua mbegu sehemu ya kubwa ya shamba hali inayowafanya kurudia kupanda mara kwa mara.

Akijibia kero hiyo katika mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kitongoji cha Kitapi Kata ya Mbwara Novemba 21, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele alisema Wataalamu watafika Wilayani Rufiji kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo.

“sasa wakija hapa hapa Kitapi, hakikisha unakuja na mafuta, fungu la dagaa na pumba za Mahindi kwaajili ya kuchanganya na dawa” alisema Gowele.

  

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa