• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

CHUO CHA VETA RUFIJI CHAFUNGULIWA RASMI, WAZAZI WAHIMIZWA KUPELEKA WANAFUNZI

Posted on: July 8th, 2024

Chuo cha Ufundi (VETA) Rufiji, kimefunguliwa rasmi kwa ajili ya kuanza kupokea Wanafunzi kwa mwaka wa 2024-2025 ili kutoa ujuzi kwa jamii inayoizunguka katika fani mbalimbali za muda mrefu na muda mfupi, huku Wazazi Wilayani Rufiji wametakiwa kuchangamkia fursa ya kupeleka vijana wao ili kupata ujuzi utakaowasaidia katika maisha yao.

Chuo hicho kilichojengwa kwa thamani ya Shilingi bilioni 2.6, kipo katika Kitongoji cha Nyandakatundu Kata ya Chemchem Mji Mdogo wa Utete Wilayani Rufiji barabara ya Utete-Nyamwage, kimefunguliwa jana Jumatatu Julai 8, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mhe. Kanali Joseph Kolombo aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, ambaye amewataka Wananchi wa Rufiji na Kibiti kupeleka Wanafunzi ili wapate ujuzi wa fani mbalimbali.

“unapoona fedha serikali imewekeza hapa fedha bilioni 2.6, inalenga vijana wa Rufiji waliomaliza sekondari pamoja msingi waweze kusoma na kupata ujuzi mbalimbali. Mimi binafsi nimechukua kama agenda katika vikao vya nitakavyokuwa nafanya ni Vijana waje kusoma hapa Rufiji” alisisitiza DC Kolombo.

Akitoa taarifa ya Chuo, Msajili wa Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Rufiji Julius Mwakasasa, amesema Chuo kimeshapokea Wananfunzi 14 mpaka sasa ambao wanasomea fani ya umeme, huku akizitaja fani za muda mrefu za mwaka mmoja zinazotolewa chuoni hapo.

“chuo kitakuwa kinatoa fani 6, fani ya mafundi wa ujenzi, uungaji wa vyuma, ubunifu na ushonaji wa mavazi, uwaziri na kompyuta, ufundi umeme wa majumbani na ufundi wa magari. kwa mwaka wa masoma 2024 chuo kimeanza kutoa mafunzo katika fani ya umeme wa majumbani kwa idadi ya Wanafunzi 14 wote wakiwa wakiume, chuo tayari kimeanza kutoa fomu za udahili kwa muhula wa 2025” alisema Mwakasasa.

Amesema kwa mwaka Chuo kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 120 wa jinsia zote wa fani za muda mrefu, huku akibanisha kwa mwaka 2025 chuo kinatarajia kuanza masomo katika fani tatu, ufundi wa ujenzi, ubunifu na ushonaji wa mavazi pamoja na ufundi wa umeme wa majumbani.

Pia alizitaja fani za muda mfupi ambazo ni pamoja na, kompyuta, ufundi wa magari, ufundi wa ushonaji wa mavazi, umeme wa majumbani, ufundi bomba, ujenzi, uungaji wa vyuma, udereva wa pikipiki na bajaji, udereva wa awali pamoja na kozi mbalimbali za ujasiliamali kama vile ufugaji na kilimo.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa