• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

BOTI MPYA MBILI (2) ZA HALMASHAURI ZAKAGULIWA

Posted on: May 2nd, 2021


Leo Mei 02. 2021 Mkuu wa Wilaya Rufiji Kanali Patrick Sawala ameshiriki Ukaguzi wa Boti mbili ( 2 ) za Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji katika Kiwanda cha Songoro Marine Transport Ltd kilichopo Kigamboni Jijini Dar es salaam, ikiwa ni hatua ya mwisho tayari kwa boti hizo kuingia ndani ya Mto Rufiji na kuanza kazi.

Katika ukaguzi huo ameambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Juma Ligomba, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Geriad Mgoba, Mweka Hazina wa Halmashauri Bi. Anthonia Ndawi pamoja na Kamati ya Ukaguzi toka Wilayani.

Boti hizo za kisasa ambazo ni Boti za uokoaji na Boti ya doria, zimegharimu jumla ya kiasi cha shilingi Milioni 90,830,000 za Kitanzania kwa kila boti moja ambapo Boti ya doria inauwezo wa kubeba watu 11 na boti ya uokoaji ina Vitanda 03, siti 03, pamoja na choo kimoja.

Akizungumza baada ya kujiridhisha na ukaguzi huo, Kanali Sawala amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji kukamilisha taratibu zote zilizobaki ndani ya wiki ijayo ili taratibu za mafunzo kwa manahodha wa boti hizo na hatimaye sherehe za kukabidhi zianze mapema ndani ya mwezi huu.

“ Watu husema Supu ya Mbwa inanywewa ikiwa ya moto. Naomba taratibu zote zikamilike ndani ya wiki ijayo ili tufanye sherehe ya makabidhiano na Wanarufiji Waanze kuzitumia mapema.” Alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Juma Ligomba amemshukuru Mmliki wa Kampuni hiyo Bw. Songoro kwa uzalendo aliouonesha kwa kutengeneza boti hizo kwa ubora wa kiwango cha juu pamoja na msaada alioutoa kwa Wanarufiji kwa kutoa Kitanda kimoja cha kusafirishia boti bila gharama yoyote.

” Kwakweli hatuna budi kukushukuru kwa niaba ya Wanarufiji. Hakika umetuonesha upendo mkubwa na uzalendo wa hali ya juu sana.” Alisema.

Akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mwenyekiti wa Kamati ya ukaguzi na Kaimu Afisa mifugo na Uvuvi Wilaya Bw. Salim Msangi amesema, boti hizo za kisasa licha ya kutumika na idara yake kwa shughuli za doria na uokoaji, Boti hizo zitakwenda kutoa huduma kwa Watalii wan je na wandani, kukodisha kwa shughuli mbalimbali, na kuongeza nguvu kwa usafiri wa majini ambapo zitaongeza kipato na kukuza utalii wilayani Rufiji.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA RUFIJI WAANZA MAFUNZO RASMI

    August 04, 2025
  • PINDA AZINDUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI MKOANI MOROGORO

    August 02, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa